1 Corinthians 15

Kufufuka Kwa Al-Masihi

1 aBasi ndugu zangu nataka niwakumbushe kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo katika hiyo mmesimama. 2 bKwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili.

3 cKwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Al-Masihi alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo Maandiko, 4 dya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko, 5 ena kwamba alimtokea Kefa,
Yaani Petro.
kisha akawatokea wale kumi na wawili.
6 gBaadaye akawatokea wale ndugu waumini zaidi ya 500 kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala. 7 hNdipo akamtokea Yakobo na kisha mitume wote. 8 iMwisho wa wote, akanitokea mimi pia, ambaye ni kama aliyezaliwa si kwa wakati wake.

9 jKwa maana mimi ndiye mdogo kuliko mitume wote, nisiyestahili kuitwa mtume, kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu. 10 kLakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo na neema yake kwangu haikuwa kitu bure. Bali nilizidi sana kufanya kazi kuliko mitume wote, lakini haikuwa mimi, bali ni ile neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami. 11 lHivyo basi, kama ilikuwa mimi au wao, hili ndilo tunalohubiri, na hili ndilo mliloamini.

Ufufuo Wa Wafu

12 mBasi kama tumehubiri ya kwamba Al-Masihi alifufuliwa kutoka kwa wafu, mbona baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu? 13Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Al-Masihi hakufufuliwa. 14 nTena ikiwa Al-Masihi hakufufuliwa kutoka kwa wafu, kuhubiri kwetu kumekuwa ni bure na imani yenu ni batili. 15 oZaidi ya hayo, twaonekana kuwa mashahidi wa uongo kuhusu Mungu, kwa sababu tumeshuhudia kumhusu Mungu kwamba alimfufua Al-Masihi kutoka kwa wafu, lakini hilo haliwezi kuwa kweli kama wafu hawafufuliwi. 16 pKwa kuwa kama wafu hawafufuliwi, basi hata Al-Masihi hajafufuka. 17 qTena kama Al-Masihi hajafufuliwa, imani yenu ni batili; nanyi bado mko katika dhambi zenu. 18 rHivyo basi, wote waliolala katika Al-Masihi wamepotea. 19 sIkiwa tumaini letu ndani ya Al-Masihi ni kwa ajili ya maisha haya tu, sisi tunastahili kuhurumiwa kuliko watu wote.

20 tLakini kweli Al-Masihi amefufuliwa kutoka kwa wafu, tunda la kwanza la wale wote waliolala. 21 uKwa maana kama vile mauti ilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja. 22 vKwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Al-Masihi wote watafanywa hai. 23 wLakini kila mmoja kwa wakati wake: Al-Masihi, tunda la kwanza kisha, wale walio wake, wakati atakapokuja. 24 xNdipo mwisho utafika, wakati atakapomkabidhi Mungu Baba ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu. 25 yKwa maana lazima Al-Masihi atawale mpaka awe amewaweka adui zake wote chini ya miguu yake. 26 zAdui wa mwisho atakayeangamizwa ni mauti. 27 aaKwa maana Mungu “ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini isemapo kwamba “vitu vyote” vimewekwa chini yake, ni wazi kwamba Mungu aliyetiisha vitu vyote chini ya Al-Masihi hayumo miongoni mwa hivyo vilivyotiishwa. 28 abAtakapokuwa amekwisha kuyafanya haya, ndipo Mwana mwenyewe atatiishwa chini yake yeye aliyetiisha vitu vyote, ili Mungu awe yote katika yote.

29Basi kama hakuna ufufuo, watafanyaje wale wabatizwao kwa ajili ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, mbona watu wanabatizwa kwa ajili yao? 30 acNasi kwa upande wetu kwa nini tunajihatarisha kila saa? 31 adKama majivuno yangu kwa ajili yenu katika Al-Masihi Isa Bwana wetu ni kweli, ndugu zangu, ninakufa kila siku. 32 aeKama kwa sababu za kibinadamu tu nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, ningekuwa nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi, “Tuleni na kunywa,
kwa kuwa kesho tutakufa.”

33 afMsidanganyike: “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 34 agZindukeni mwe na akili kama iwapasavyo, wala msitende dhambi tena; kwa maana watu wengine hawamjui Mungu. Nasema mambo haya ili mwone aibu.

Mwili Wa Ufufuo

35 ahLakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?” 36 aiNinyi wapumbavu kiasi gani? Mpandacho hakiwi hai kama hakikufa. 37Mpandapo, hampandi mwili ule utakao kuwa, bali mwapanda mbegu tu, pengine ya ngano au ya kitu kingine. 38 ajLakini Mungu huipa mbegu umbo kama alivyokusudia mwenyewe na kila aina ya mbegu huipa umbo lake. 39Kwa maana nyama zote si za aina moja. Binadamu wana nyama ya aina moja, wanyama wana aina nyingine, kadhalika ndege na samaki wana nyama tofauti. 40Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani, lakini fahari wa ile miili ya mbinguni ni wa aina moja na fahari wa ile miili ya duniani ni wa aina nyingine. 41 akJua lina fahari ya aina moja, mwezi nao una fahari yake na nyota pia, nazo nyota hutofautiana katika fahari.

42 alHivyo ndivyo itakavyokuwa wakati wa ufufuo wa wafu. Ule mwili wa kuharibika uliopandwa, utafufuliwa usioharibika, 43 amunapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu, unapandwa katika udhaifu, unafufuliwa katika nguvu, 44 anunapandwa mwili wa asili, unafufuliwa mwili wa kiroho.

Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia.
45 aoKwa hiyo imeandikwa, “Mtu wa kwanza Adamu alifanyika kiumbe hai”; Adamu wa mwisho, yeye ni roho iletayo uzima. 46Lakini si ule wa kiroho uliotangulia, bali ni ule wa asili, kisha ule wa kiroho. 47Mtu wa kwanza aliumbwa kwa mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni. 48 apKama vile alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na kwa vile alivyo mtu yule aliyetoka mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni. 49 aqKama vile tulivyochukua mfano wa mtu wa ardhini, ndivyo tutakavyochukua mfano wa yule mtu aliyetoka mbinguni.

50 arNdugu zangu nisemalo ni hili: nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika. 51 asSikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa 52 atghafula, kufumba na kufumbua, parapanda ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa parapanda italia, nao wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa. 53 auKwa maana mwili huu wa kuharibika lazima uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa lazima uvae kutokufa. 54 avKwa hiyo, mwili huu wa kuharibika utakapovaa kutokuharibika, nao huu mwili wa kufa utakapovaa kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia: “Mauti imemezwa kwa kushinda.”
55 aw“Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako?
Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?”

56 axUchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria. 57 ayLakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Isa Al-Masihi.

58 azKwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana si bure.
Copyright information for SwhKC